Wenger aomba msamaha baada ya kumsukuma Mourinho.
Kocha wa klabu ya Arsenal,Arsene Wenger ameomba radhi kwa kitendo chake cha kumsukuma kocha wa Chelsea Jose Mourinho katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliopigwa Octoba 5 katika uwanja wa Stamford Bridge."Watu wameipa sana kipaumbele tukio hili lakini sijawahi kufanya tukio kama hili katika soka. Ninajutia kwa tukio nililofanya na ninaomba msamaha," Wenger aliimbia runinga ya taifa ya Ufaransa TF1.
Wenger alikwenda kumsukuma Mourinho sehemu ya kifua chake katika mchezo huo uliomalizika kwa Chelsea kushinda mabao 2-0 October 5 mwaka huu.
Akizungumza na TF1, Mourinho amesema ''sitazungumzia chochote. Sina la kuongezea katika picha ambazo dunia imeshuhudia''.
0 comments:
Post a Comment