Kluivert atemwa kwa wanaowania ukocha Ghana,Shuster aitwa.
Majina ya makocha yaliyobaki ni kocha wa zamani wa Chelsea Avram Grant,kiungo wa zamani wa Italy Marco Tardelli, mswisi Michel Pont na mhispania Juan Ignacio Jimenez.
"Pont na Tardelli watafanyiwa usaili mjini Accra October 17, wakati Grant na Jimenez wataenda October 18," imesema GFA.
Nyota huyo wa zamani wa Real Madrid , Schuster, ataitwa ili kufanya usaili ndani ya siku hizo.
Schuster ni baadhi ya wachezaji wachache waliong'ara na Real Madrid na kujiunga na watani wa jadi Barcelona, na kushinda mataji.
Alisaidi Ujerumani kubeba ubingwa wa ulaya mwaka 1980, baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Ubelgiji katika fainali.

0 comments:
Post a Comment