EPL kuendelea tena kesho,Liverpool na Chelsea kupepetana.
Ligi kuu ya kandanda nchini Uingereza itaendelea tena Jumamosi hii ambapo mechi ya mapema itakuwa katika uwanja wa Anfield kati ya Liverpool na Vinara wa Ligi Chelsea.Mechi hii, itakayoanza Saa 9 Dakika 45 alasiri, inazikutanisha Liverpool, walio Nafasi ya 7 kwenye Ligi, na Vinara wa Ligi Chelsea walio alama 12 mbele yao.
Ikumbukwe kuwa Timu zote hizi mbili zinatoka kwenye Mechi za ligi ya mabingwa barani Ulaya wakati Liverpool, ilifungwa 1-0 huko Hispania na Mabingwa wa Ulaya Real Madrid na Chelsea kucheza ugenini huko Slovenia na kutoka 1-1 na NK Maribor.
Kwenye Ligi, Wikiendi iliyopita, Liverpool ilichapwa 1-0 na Newcastlle na Chelsea kuifunga QPR Bao 2-1.
Msimu uliopita, kwenye Mechi kama hii, Chelsea iliitwanga Liverpool mabao 2-0.
Ratiba Jumamosi Novemba 8,mechi zote kwa saa za Tanzania.
Liverpool v Chelsea 1545
Burnley v Hull 1800
Man United v Crystal Palace 1800
Southampton v Leicester 1800
West Ham v Aston Villa 1800
QPR v Man City 2030
Jumapili Novemba 9
Sunderland v Everton 1630
Tottenham v Stoke 1630
West Brom v Newcastle 1630
1900 Swansea v Arsenal
0 comments:
Post a Comment