Toure aomba radhi baada ya kupewa kadi nyekundu.

Mabao mawili yaliyofungwa na Seydou Doumbia yaliipa CSKA ushindi wao wa kwanza nchini Uingereza, wakati klabu hiyo ikishuhudia Fernandinho akipewa kadi mbili za njano katika kipindi cha pili na Toure kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumsukuma Roman Eremenko.
Matokeo hayo yanaifanya City ambao hawajashinda mechi hata moja kushika mkia katika kundi E na kuwaacha katika hatari ya kutolewa huku wakiwa wamebaki na mechi mbili dhidi ya Bayern Munich na AS Roma.
Toure aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akiwaomba radhi mashabiki kwa kadi hiyo aliyopata pamoja na matokeo.
Mbali na Toure Fernandinho naye aliomba radhi kwa kupata kadi ya pili ya njano ambayo ilisabababisha kikosi chao kuelemewa na kupoteza mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment