Monday, 17 November 2014

Federer ajitoa katika michuano ya ATP.

Mcheza tenis Roger Federer amejiondoa kwenye Fainali ya michuano ya dunia ya ATP ambapo alikua anatarajiwa kuchuana na Novak Djokovic. 

Taarifa zinaeleza kuwa  chanzo cha kujitoa ni maumivu ya mgongo aliyokua akiyapata.

Mswiss huyo alijitokeza hadharani kwenye uwanja wa 02 Arena mwenyewe na kutangaza kuwa hayuko tayari kucheza .

Ikumbukwe kuwa siku ya jumamosi Federer alimshinda Stan Wawrinka kwa 4-6 7-5 7-6(8-6) katika mchezo wa kusisimua wa nusu fainali ambao ulichezwa kwa saa mbili na dakika 48.

0 comments:

Post a Comment