Ulingo wa mieleka John Cena amchapa Randy Orton,Big Show achapwa na Rusev.

Mwezi mzima ulitawaliwa na maneno ya hapa na pale kutoka kwa wanamieleka huku kila moja akitamba kuwa atamshinda mwenzake.
Mpambano uliokuwa unasubiriwa kwa hamu ni ule kati ya John Cena na Randy Orton ambapo mshindi atacheza na Brock Lesner.
Hatimaye John Cena alitamba kwa mara nyingine baada ya kumpiga mzee wa RKO,Rand Orton na hivyo Cena atapigana na Brock Lesnar ili kugombania ubingwa wa dunia.
Matoke mengine.
Seth Rollins alimpiga Dean Ambrose (Hell in a Cell )
Rusev alimgaragaza Big Show
Bingwa wa United States Sheamus alitetea taji lake kwa kumpiga The Miz
Mabingwa wa dunia katika mchezo wa timu iliyoungana Gold & Stardust walishinda mbele ya The Usos
Bingwa kwa upande wa akina dada maarufu kama Divas Champion AJ Lee alimpiga Paige
Bingwa wa mabara Dolph Ziggler alishinda mbele ya Cesaro
Mark Henry alimpiga Bo Dallas
0 comments:
Post a Comment