Thursday, 20 November 2014

Zifahamu Nchi 16 zilizofuzu AFCON 2015,Nigeria Out.

Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, ambazo zitachezwa kuanzia Januari 17, tayari zimeshapata Washiriki 15 watakaojumuika na Wenyeji Equatorial Guinea baada ya Mechi za mwisho za Makundi hapo Jana.

Lakini Mabingwa Watetezi Nigeria wameshindwa kufuzu baada ya kutoka Sare 2-2 na Afrika Kusini  kutoka Kundi A huku Congo Brazzaville ikipita baada ya kuifunga Sudan 1-0 huko Khartoum.

Kila Kundi limetoa Timu mbili kufanya Jumla ya Timu 14 na ya 15 ni ile iliyomaliza Nafasi ya 3 Bora toka Kundi lake ukilinganisha na nyingine za Nafasi hiyo.

NCHI ZILIZOFUZU KUINGIA FAINALI AFCON 2015:

Equatorial Guinea amefuzu kama Mwenyeji

Kutoka kundi  A: South Africa, Congo

Kundi B: Algeria, Mali

KundiC: Burkina Faso, Gabon

Kundi D: Cameroon, Ivory Coast

KundiE: Ghana, Guinea

Kundi F: Cape Verde, Zambia

KundiI G: Tunisia, Senegal

Nchi ya Congo DR imeingia kama mshindi wa tatu bora

FAINALI kuchezwa kuanzia Januari 17 hadi Februari 8

0 comments:

Post a Comment