Kolo,Yaya Toure na Bony watajwa kikosi cha Ivory Coast AFCON 2015
Mchezaji Kolo Toure ameitwa katika kikosi cha wachezaji 23 wa timu ya taifa ya Ivory coast Kitakachoshiriki michuano ya AFCON hapo mwakani.Mlinzi huyo wa Liverpool, 33, amesema kuwa ataachana na tembo hao baada ya michuano hiyo ambayo itaanza kunguruma Januari 17 hadi Februari 8 nchini Equatorial Guinea.
Kaka yake, kiungo wa Manchester City Yaya, pia amejumuishwa.
Nyota wa Swansea Wilfried Bony na nyota wa Newcastle Cheick Tiote ni wachezaji walioitwa wanaocheza Katika EPL.
Michezo ya Ivory Coast katika kundi D.
20 Jan: v Guinea
24 Jan: v Mali
28 Jan: v Cameroon
KIKOSI KAMILI
Makipa: Gbohouo Sylvain (Sewe), Mande Sayouba (Staebek), Coppa Barry (Lokeren)
Walinzi: Aurier Serge (PSG), Tiene Sakia (Montpelier), Viera Ousmane (Rizesport), Kolo Toure ( Liverpool), Wilfried Kanon (ADO), Eric Bertrand Bailly (Espanyol), Akpa Akpro Jean-Daniel (Toulouse)
Viungo: Diomande Ismael (St Etienne), Yaya Toure (Manchester City), Serey Die Geoffrey (Bâle), Doukouré Cheick (Metz), Cheick Tiote (Newcastle) Gradel Max (St Etienne), Assale Roger (Sewe San Pedro)
Washambuliaji: Gervinho (AS Roma), Kalou Salomon (Hertha Berlin), Traore Lacina (Monaco), Tallo Junior (Bastia), Wilfried Bony (Swansea), Seydou Doumbia (CSKA Moscow)

0 comments:
Post a Comment