Thursday, 29 January 2015

FIFA YACHUNGUZA TUHUMA ZA UPANGAJI MATOKEO

Ujumbe wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) upo nchini kuchunguza tuhuma za upangaji matokeo.

Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa mashindano ya TFF  Boniface Wambura imeeleza kuwa Waamuzi waliosimamishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu  Tanzania (TFF) pamoja na watu wengine watahojiwa na ujumbe huo. Matokeo ya uchunguzi huo yatatangazwa na FIFA baada ya shughuli hiyo kukamilika.

TFF inaendelea  kuwahimiza wanafamilia wa mpira wa miguu wazidi kuzingatia kanuni za maadili za TFF, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na FIFA katika utendaji wao.

FIFA itahakikisha kuwa haki inatendeka katika uchunguzi ambao inaufanya.

0 comments:

Post a Comment