Friday, 2 January 2015

Gerrard kuondoka ndani ya Liverpool mwishoni mwa msimu huu

Nahodha wa klabu ya Liverpool, Steven Gerrard ametaja uamuzi wake wa kuondoka katika timu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Gerrard mwenye umri wa miaka 34 anatarajia kumaliza mkataba wake katika majira ya kiangazi baada ya kujiunga na klabu hiyo akiwa na miaka tisa na kufunga mabao 180 katika mechi 695 alizowahi kuichezea Liverpool.

Akihojiwa na wanahabari Gerrard amesema uamuzi huo ni mgumu kuwahi kufanya katika maisha yake na ameamua kufanya uamuzi huo  yeye pamoja na familia yake wamekuwa wakiuandaa kwa kipindi kirefu.

Kiungo huyo aliendelea kudai kuwa anaweza kuendelea kucheza lakini haitakuwa katika timu ambayo inayoweza kukutana na Liverpool katika mechi zake.

Gerrard anahisishwa na kuhamia katika Ligi Kuu nchini Marekani-MLS mara baada msimu wao soka Uingereza utakapomalizika.

0 comments:

Post a Comment