Friday, 2 January 2015

VPL kuendelea kesho,Ruvu Shooting na Kagera Sugar.

Ligi kuu soka Tanzania bara itaendelea kunguruma kesho(Januari 3 mwaka huu) katika mechi ya raundi ya 9.

Kwa mujibu wa ratiba   Wagosi wa Kaya, Coastal Union watawakaribisha Maafande wa JKT Ruvu uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga.

Wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 katika mechi iliyopita dhidi ya JKT Ruvu,  Maafande wa Ruvu Shootings watawaalika ‘Wanankurukumbi’ Kagera Sugar FC kwenye uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani.

Polisi Morogoro watakabiliana na Stand United katika uwanja wa michezo wa Jamhuri uliopo mjini Morogoro.

Jumapili januari 4 mwaka huu, Nyasi za uwanja wa CCM Sokoine zitawaka moto kwa wenyeji Tanzania Prisons, kuchuana na Ndanda fc.

Mechi baina ya Mbeya City fc na Yanga, Azam fc dhidi ya Mtibwa Sugar pamoja na ile ya Mgambo na Simba zimeahirishwa kwani Yanga, Simba, Azam na Mtibwa zipo Zanzibar.

0 comments:

Post a Comment