Friday, 2 January 2015

Gerrard kutoa kauli leo kuhusu Liverpool,Jamie Carragher Asema ni sawa tu.

Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard leo ijumaa anatarajia kutangaza kumaliza miaka yake 26 ya kuichezea Liverpool.

Nyota huyu aliyedumu ndani ya  Anfield anatarajia kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Gerrard aliyejiunga na klabu hiyo akiwa na miaka 8 tu anatakiwa na klabu ya  LA Galaxy.

Hata hivyo, Gerrard amesisitiza kuwa hajafikia maamuzi yoyote na klabu yake.

Kiungo huyu mahiri ameachana na  mpango wa kuongeza Mkataba Anfiedl na amekuwa huru kuzungumza na klabu nyingine kutoka jana januari mosi mwaka huu.

Wakati hayo yakiendelea nyota wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher amekubaliana na hali ya Gerard kuondoka Anfield.


0 comments:

Post a Comment