Ligi daraja la kwanza,Polisi Tabora na Geita,Toto na Panone,Mwadui mhhhhh
Klabu ya Polisi Tabora itapambana na Geita Gold ya mkoani Geita leo(Januari 21) katika mchezo wa ligi daraja la kwanza.
Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kuanzia saa kumi na nusu jioni hii huku Polisi Tabora Ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 2-1 na Toto Afrika ya Mwanza katika mchezo uliopita.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo Bernard Fabian Adam amesema kuwa vijana wamejiandaa vema ili kushinda mpambano huo huku akiahidi ushindi kwa washabiki wa soka wa Klabu hiyo.
Kule Shinyanga Rhino Rangers Tabora itakuwa mgeni wa Mwadui FC katika mchezo ambao utapigwa Mkoani Shinyanga.
Katika mchezo wake wa mwisho Rhino Iliibuka na Ushindi wa 3-0 dhidi ya Green Warrious ya Dar es salaam.
Kule Moshi Panone watakuwa wenyeji wa Toto Africa ya Mwanza,Toto inahitaji ushindi ili ijikite kileleni mwa kundi lao.
Timu hizi zipo Kundi B ambalo linaongozwa na Toto African yenye alama 35 ikifuatiwa na Mwadui FC ambayo ina alama 32 ,JKT Oljoro ina alama 29, Polisi Tabora alama 26 na Rhino alama 25.

0 comments:
Post a Comment