Saturday, 3 January 2015

Pardew rasmi Crystal Palace.

Kocha wa zamani  wa Newcastle United Alan Pardew ameanza kazi rasmi kuwa kocha wa Crystal Palace.

Pardew alipewa ruksa ya kufanya mazungumzo na Palace huku klabu hizo mbili zikikubaliana kugawana gharama za kuvunja mkataba wake.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 53 anachukua nafasi ya Neil Warnock ambaye ametimuliwa Jumamosi iliyopita ikiwa ni imepita miezi minne toka apewe timu hiyo kwa mara ya pili.

Palace haijathibitisha rasmi suala hilo lakini inafahamika kuwa Pardew alisaini mkataba na timu hiyo jana jioni.

0 comments:

Post a Comment