Matokeo VPL,Coastal Union yatulizwa,Kagera na Ruvu hakuna mbabe.
Klabu ya Polisi Morogoro imelazimishwa suluhu na Stend United ya Shinyanga katika uwanja wake wa nyumbani katika mfulululizo wa ligi kuu ya Tanzania VPL.Kwa matokeo hayo Polisi imefikisha alama 13 huku Stendi ikifikisha alama 11.
Mchezo huo ulishuhudiwa kwa mchezaji Haruna Chanongo kupewa kadi nyekundu mnamo dakika ya 84 ya mchezo baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano baada ya kuzozona na mwamuzi msaidizi.
Matokeo mengine
Coastal Union 0 JKT Ruvu 1
Ruvu Shooting 0 Kagera Sugar 0
Kesho Jumapili januari 4 mwaka huu, Nyasi za uwanja wa CCM Sokoine zitawaka moto kwa wenyeji Tanzania Prisons, kuchuana na Ndanda fc.
Mechi baina ya Mbeya City fc na Yanga, Azam fc dhidi ya Mtibwa Sugar pamoja na ile ya Mgambo na Simba zimeahirishwa kwani Yanga, Simba, Azam na Mtibwa zipo Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment