Real Madrid klabu tajiri duniani,ikifuatiwa na Manchester United.
Klabu ya Real Madrid wamekuwa kileleni mwa Listi ya Klabu Tajiri Duniani kwa miaka 10 mfululizo.Kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa Jana na Deloitte, ambao ni Wataalam wakubwa wa Mahesabu Duniani.
Katika orodha hiyo Manchester United wamepanda kutoka Nafasi ya 4 na kushika Nafasi ya Pili katika Msimamo uliochukulia Mapato ya Mwaka 2013/14 kama ndio kigezo.
Baada ya Man United, Klabu zinazofuatia kwenye Listi hiyo ya Utajiri Duniani ni Bayern Munich, Barcelona na Paris Saint-Germain kisha Klabu za Uingereza Manchester City, Chelsea, Arsenal na Liverpool.
Listi hii, ambayo imesheheni Klabu za Ligi kubwa Ulaya, haikuangalia nini Madeni ya Klabu.
KUMI BORA.
1. Real Madrid: 549.5m (518.9m)
2. Man Utd: 518m (423.8m)
3. Bayern Munich: 487.5m (431.2m)
4. Barcelona: 484.6m (482.6m)
5. Paris Saint Germain; 474.2m (398.8m)
6. Manchester City: 414.4m (316.2m)
7. Chelsea: 387.9m (303.4m)
8. Arsenal: 359.3m (284.3)
9. Liverpool: 305.9m (240.6m)
10. Juventus: 279.4m (272.4m)
0 comments:
Post a Comment