Rhino na Polisi Dodoma,Toto na Polisi Tabora,ni katika FDL.
Klabu ya Rhino Rangers ya hapa mkoani Tabora itapambana na Polisi Dodoma leo katika mchezo wa ligi daraja la kwanza.
Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kuanzia saa kumi na nusu jioni hii huku Rhino Ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 na Panone ya Moshi katika mchezo uliopita.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo Didas Kunde amesema kuwa vijana wamejiandaa vema ili kushinda mpambano huo huku akiahidi ushindi kwa washabiki wa soka wa Klabu hiyo.
Kule mwanza Polisi Tabora itakuwa mgeni wa Toto Afrika katika mchezo ambao utapigwa katika uwanja wa CCM Kirumba.
Katika mchezo wake wa mwisho Polisi Tabora Iliibuka na Ushindi wa 1-0 dhidi ya Burkinafaso ya Morogoro.
Timu hizi zipo Kundi B ambalo linaongozwa na Mwadui FC yenye alama 30 ikifuatiwa na Toto African,JKT Oljoro, Polisi Tabora zenye alama 26 kila mmoja
0 comments:
Post a Comment