Kipande cha kombe la dunia lililoibwa chapatikana.
Kipande cha taji la Kombe la Dunia halisi ambalo liliibiwa nchini Brazil mwaka 1983 na kutowahi kupatikana, kimepatikana katika chumba cha chini katika makao makuu ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA yaliyopo jijini Zurich, Switzerland.Taji hilo ambalo zamani lilikuwa likiitwa Jules Rimet, lilipatikaan sehemu ya chini ambayo bado ilikuwa na majina ya mabingwa wanne wa kwanza wa Kombe la Dunia ambao ni Uruguay walionyakuwa taji hilo mwaka 1930 na 1950 na Italia mwaka 1934 na 1938.
Taji ambalo walipewa Brazil moja kwa moja baada ya kushinda Kombe la Dunia kwa mara tatu mwaka 1970 pia liliibiwa miezi mitatu kabla ya michuano hiyo mwaka 1966 iliyofanyika nchini Uingereza
0 comments:
Post a Comment