Tuesday, 27 January 2015

Simba yalimwa adhabu na TFF.

Klabu ya Simba italimwa faini na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kutopeleka timu uwanjani wakati wa mechi yao iliyopita dhidi ya Azam FC.

Simba haikupeleka kikosi B kumenyana na kikosi B cha Azam FC kabla ya kuanza kwa mechi yao ya raundi ya 12 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana.

Humphrey Nyasio, msemaji wa Simba, amesema kuwa wamefanya kosa hilo kutokana na "matatizo ya ndani ya uongozi wa klabu."

Nyasio amesema kuwa  timu ya  vijana haikuingia uwanjani  kwa sababu haikufanya mazoezi wiki iliyopita kutokana na matatizo ya ndani ya uongozi ambayo haiapewa ruhusa ya kuyazungumzia kwa sasa.

Simba itapigwa faini ya Sh. 500,000 na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) kwa kutopeleka kikosi B uwanjani, kwa mujibu wa Kanuni za Ligi za TFF toleo la 2014.

0 comments:

Post a Comment