Leo vita ya Ghana na Afrika kusini,Algeria na Senegal.
Timu za taifa za Ghana na Afrika kusini zinapamba leo usiku katika mechi za mwisho za makundi ya kombe la mataifa barani Afrika nchini Equatorial Guinea.
Kuelekea mchezo huo kocha wa Afrika ya kusini Shakes Mashaba amesema leo lazima timu yake ishinde ili kuhakikisha wanaingia hatua ya robo fainali.
Afrika ya kusini Ilifungwa mabao 3-1 na Algeria kabla ya kutoka sare ya 1-1 na Senegal,hivyo wanahitaji kushinda dhidi ya Ghana.
Kocha wa Ghana Avram Grant alipoteza mchezo wa ufunguzi kwa 2-1 dhidi ya Senegal kabla ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Algeria kwa bao la Asamoah Gyan.
Afrika ya kusini itawategemea washambuliajhi Bongani Ndulula na Tokelo Rantie huku mlinzi Brilliant Khuzwayo akipewa jukumu la kuwadhibiti washambuliaji wa Ghana.
Ghana itamtegemea zaidi nyota Asamoah Gyan katika nafasi ya ushambuliaji.
Vilevile hii leo Algeria itapambana na Senegal mechio za kundi C.
Iwapo Ghana ikishinda itafikisha alama 6 na kuziba nafasi ya bafanabafana kufuzu lakini bafanabafana nao wakishinda watafikisha alama 4 lakini wana nafasi ngumu ya kusonga mbele.
Ikiwa Algeria na Senegal zitatoka sare huku Ghana wakifungwa basi zitafuzu hatua ya robo fainal.
0 comments:
Post a Comment