Ligi daraja la kwanza leo ni Polisi Mara na Polisi Tabora.
Ligi daraja la kwanza itaendelea kunguruma leo kwa mchezo moja ambapo Timu za Polisi Tabora na Polisi Mara zitapambana katika uwanja wa Karume mjini musoma.Mechi hii ni kiporo baada ya kuahirishwa kuchezwa kutokana na uwanja wa Karume mjini Musoma kufungiwa na bodi ya ligi.
Mchezo huo utapigwa kuanzia saa kumi na nusu jioni huku Polisi Tabora ikiahidi ushindi.
Kocha msaidizi wa Polisi Tabora Bernard Fabiana Adam amesema mchezo huo utakuwa mgumu kwao huku wakihitaji ushindi ili kupata nafasi ya kushiriki ligi kuu.
Ameeleza kuwa timu ina ari kubwa huku mchezo wa mwisho walishinda bao 1-0 dhidi ya JKT Kanembwa
Mechi za raundi ya 21 kundi B Zitaanza Februari 10 mwaka huu na mechi hizo ni Burkina Faso vs JKT Kanembwa, Mwadui vs Polisi Tabora, Polisi Dodoma vs Green Warriors, Rhino Rangers vs JKT Oljoro, Panone vs Polisi Mara, Geita Gold vs Toto Africans.
Raundi ya 22 itachezwa Februari 15 mwaka huu kwa mechi kati ya JKT Kanembwa vs Green Warriors, Mwadui vs Burkina Faso, Polisi Tabora vs JKT Oljoro, Polisi Dodoma vs Panone, Toto Africans vs Rhino Rangers, na Geita Gold vs Polisi.
Kundi hilo linaongozwa na Mwadui alama 40 wakifuatiwa na Toto alama 39,JKT Oljoro alama 35 huku Polisi Tabora ikishikilia nafasi ya nne kwa alama zao 35.
0 comments:
Post a Comment