VPL kuendelea kesho Ruvu Shooting na Polisi Morogoro.
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)itaendelea kesho siku ya
jumanne katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, wenyeji timu ya Polisi Morogoro
watawakaribisha Ruvu Shooting kutoka Mlandizi mkoani Pwani.
Siku ya jumatano JKT Ruvu watawakaribisha Young Africans
katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku jijini Tanga Mgambo Shooting
wakiwa wenyeji wa timu ya Azam FC.
Aidha mechi ya
Kombe la Shirikisho (CC) barani Afrika kati ya Young Africans dhidi ya timu ya
FC Platinum ya Zimbabwe, itafanyika siku ya jumapili Machi 15, 2015 katika
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment