Kanu asema Supe Eagles si wazuri kwa sasa.
Nyota wa zamani wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Nigeria Kanu Nwankwo amesisitiza kuwa timu ya taifa ya Nigeria si nzuri ila amesema itakuja kuwa nzuri muda si mrefu.
Nigeria maarufu kwa jina la Super Eagles haipati matokeo mazuri tokea watwae ubingwa wa Afrika mwaka 2013.
Kanu amesema kuwa kushindwa kufuzu mashindano ya AFCON mwaka 2015 kule Equatorial Guinea si picha nzuri ila anaamini kuwa timu itakuwa nzuri siki zijazo.
Nyota huyo aliyewahi kuzichezea pia Ajax na Inter Milan ameongeza kuwa mgogoro wa soka nchini kwao lazima uwekwe wazi ili timu ipate matokeo mazuri.
Kanu aliyechezea Nigeria mechi 87 tokea 1994 hadi 2011 ameongeza kuwa hafurahishwi na mgogoro unaoendelea nchini mwake.
0 comments:
Post a Comment