Michuano ya Miami Open yafikia nusu fainali.
Mcheza tenis wa Uingereza Andy
Murray amefanikiwa kuingia nusu fainali baada ya kumshinda Dominic Thiem
raia wa Austria katika mashindano ya Miami Open yanayoendelea huko
nchini Marekani.
Murray mwenye umri wa miaka 27, anaweza kupambana na Tomas Berdych raia wa Czech ama Muajentina Juan Monaco katika nusu fainali ya mashindano hayo.
Naye Serena Williams amepata ushindi wa 700 tangu aanze kucheza mchezo huo baada ya kuingia nusu fainali kwa kumbwaga mjerumani Sabine Lisicki.
Chanzo BBC.
0 comments:
Post a Comment