Kocha bora wa mwezi EPL kuna Wenger,Van Gaal,Sherwood na Koeman.
Kocha wa klabu ya Manchester United mholanzi Louis van Gaal ametajwa kuwania tuzo za kocha bora wa mwezi katika ligi kuu Uingereza.
Katika mwezi Machi klabu ya Manchestert United imekusanya alama tisa katika mechi muhimu,mechi hizo ni ya Tottenham Katika dimba la Old Trafford na Liverpool katika uwanja wa Anfield.
Katika mwezi Machi klabu ya Manchestert United imekusanya alama tisa katika mechi muhimu,mechi hizo ni ya Tottenham Katika dimba la Old Trafford na Liverpool katika uwanja wa Anfield.
Timu hiyo inashikilia nafasi ya nne katika msimamo.
.
Makocha wengine waliotajwa ni pamoja na Arsene Wenger wa Arsenal , Tim Sherwood wa Aston Villa na Ronald Koeman. Southampton.
Washika bunduki Arsenal wameshinda mechi zao zote nne ndani ya mwezi Machi na kushikilia nafasi ya tatu nyuma ya Manchester City.
Sherwood alianza kibarua ndani ya Villa Park baada ya Paul Lambert kutimuliwa amekusanya alama sita na kuiondoa Villa katika mstari wa kushuka daraja.
Koeman, ameipa Southampton alama 7 katika mechi tatu sambamba na sare dhidi ya vinara Chelsea Uwanja wa Stamford Bridge.
Mshindi atatangazwa kesho.
0 comments:
Post a Comment