TIMU ya Taifa ya Malawi (Flames) inatarajiwa
kuwasili nchini Mei 1 mwaka huu kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa
Stars itakayochezwa Mei 4 mwaka huu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine
jijini Mbeya.
Taarifa ya TFF imeeleza kuwa Flames yenye msafara wa 31 utakaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Chama cha Mpira wa Miguu cha Malawi (FAM) utaingia Mbeya kwa usafiri wa
barabara. Wachezaji katika msafara huo ni 20
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager ikiwa chini ya Kocha mpya, Mart Nooij tayari ipo jijini Mbeya
kujiwinda kwa mechi hiyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mashindano
dhidi ya Zimbabwe itakayochezwa jijini Dar es Salaam kati ya Mei 16 na 18 mwaka
huu.
0 comments:
Post a Comment