Nahodha
wa Timu ya taifa ya Burundi Intamba
mu Rugamba , Didier Kavumbangu amesaini Mkataba wa MWAKA MOJA na mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC mchana wa leo.
Kavumbangu aliyemaliza Mkataba wake wa miaka miwili Yanga SC, ameamua kusaini
Azam FC baada ya kuona klabu yake haina mawasiliano naye licha ya kumaliza
Mkataba wake.
Akiongea
na mtandao huu kwa njia ya simu jioni ya leo afisa habari wa Azam Jafa Iddi amekiri kuwa Kavumbagu amekubali kusaini mkataba huo na kuichezea Azam katika michezo ya ligi kuu na Klabu bingwa Afrika msimu ujao.
Kavumbagu mwenyewe amekiri na kusema kuwa mpira ni kazi yake.
“Mimi
ni mchezaji, kazi yangu ni mpira. Nimemaliza mkataba Yanga, lakini viongozi
hawaniambii kitu, nimepata ofa nzuri Azam nikaamua kusaini,” amesema Kavumbangu
akizungumza baada ya kusaini Mkataba huo
Pamoja
na hayo, Kavumbangu ameishukuru Yanga SC na mashabiki kwa miaka miwili
aliyoichezea timu hiyo na anasema itabakia kwenye kumbukumbu zake kwa ameshinda
nayo mataji.
Mshambuliaji huyo amesema sasa akili yake anaipeleka kwa mwajiri wake mpya,
Azam FC ambako pia amepania kwenda kushinda mataji na kuiwezesha timu hiyo
kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika.
“Mimi sasa ni mchezaji wa Azam, nafurahi kujiunga na klabu hii kubwa. Kawaida
yangu huwa nashabikia klabu nayochezea, sasa mimi ni mshabiki namba moja wa
Azam,”amesema.
Kavumbangu
alitua Yanga mwaka 2013 akitokea Atletico ya Burundi na katika mechi misimu
miwili ya kuichezea klabu hiyo, amefunga mabao 31 katika mechi 63 za mashindano
yote, moja tu la penalti.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa mtandao huu pamoja na Bin zubeiry.
0 comments:
Post a Comment