NBA wamfungia maisha mmiliki wa Los Angeles Clippers
April 30 2014
Kamishna wa Chama cha Mpira wa Kikapu nchini Marekani bwana Silver (NBA) amemfungia maisha bwana Donald Sterling kujihusisha na Clippers au NBA, adhabu hiyo ilitangazwa siku ya Jumanne kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Manhattan.
Bwana Silver pia amempiga faini
bwana Sterling ya dola milioni 2.5, kiwango cha juu kabisa kinachoruhusiwa na
Katiba ya NBA.
Pesa hizo za faini zitatolewa kama
msaada kwenye mashirika yanayopingana na ubaguzi na juhudi za uvumilivu ambazo
zitaungana na kuchaguliwa na NBA na
Chama cha Wachezaji. Ikiwa ni adhabu
ya maisha, Sterling hatohudhuria mechi au mazoezi ya NBA, kuwepo kwenye ofisi
au miradi ya Clippers au kushiriki kwenye biashara au maamuzi ya mchezaji
yanayohusiana na timu.
Pia hatoruhusiwa kuhudhuria kwenye
vikao vya Bodi ya Magavana na kushiriki kwenye shughuli zozote za ligi.
Kamishna Silver pia alitangaza
kwamba ataihimiza Bodi ya Magavana kutekeleza uongozi wake kulazimisha kuuzwa
kwa timu.
Adhabu hiyo ilitolewa siku ya
Jumanne kutokana na maamuzi ya Kamishna huyo kwamba Sterling alikiuka sheria za
ligi kwa kutoa kauli chafu na za kuumiza, na athari yake kuonekana kwa kiasi
kikubwa kwenye ligi nzima.
Karatasi ya taarifa hiyo ambayo
Kamishna Silver aliitumia wakati wa mkutano na waandishi wa habari imetolewa
leo mchana na kutumwa kwenye mtandao wa NBA.
Chanzo ;Taarifa News

0 comments:
Post a Comment