Monday, 28 April 2014

Suarez na Hazard wang'ara tuzo za Uingereza.

Mchezaji Luis Suarez ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka Chama cha Wachezaji wa Kulipwa England jana baada ya kufunga mabao 30 msimu huu wa Ligi Kuu na kuisaidia timu yake, Liverpool kuongoza mbio za ubingwa.

Wazi tuzo hiyo inakuja kupoza machungu ya mchezaji huyo anayevalia jezi namba saba baada ya misimu iliyopita kufungiwa kwa kumkashifu Patrice Evra mwaka 2011 na kusababisha mzozo mkubwa msimu uliopita alipofungiwa mechi 10 kwa kumng'ata beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic.

Akiwa amekosa mwezi wa kwanza wa msimu huu akitumikia adhabu hiyo, Suarez alirejea Liverpool mwishoni mwa September nmwaka jana na kuunda pacha kali la ushambuliaji kwa pamoja na Daniel Sturridge.
Wanasoka bora Uingereza mwaka 2014
Mchezaji Bora wa Mwaka: Luis Suarez (Liverpool).
Mchezaji Bora Chipukizi wa mwaka: Eden Hazard (Chelsea).
Mchezaji Bora wa kike wa Mwaka: Lucy Bronze (Liverpool Ladies).
Mchezaji Bora chipukizi wanawake: Martha Harris (Liverpool Ladies).

0 comments:

Post a Comment