Droo klabu bingwa na kombe la shirikisho Afrika ni kesho
Hatimaye droo za kupanga Makundi ya kombe la klabu bingwa
Barani AFRIKA na Kombe la Shirikisho
itafanyika Jumanne Aprili 29 huko Makao Makuu ya CAF Jijini Cairo Nchini
Misri.
Kwenye CAF CHAMPIONZ LIGI zipo Timu 8 zilizofuzu
hatua hii na Droo hiyo itapanga Makundi mawili ya Timu 4 kila moja ambayo
yatacheza mtindo wa Ligi, Nyumbani na Ugenini, ili kupata Timu mbili za juu
toka kila Kundi kucheza Nusu Fainali.
Timu hizo 8 ni:
Al-Ahly Benghazi ya Libya
Al-Hilal ya Sudan
AS Vita Club ya Congo DR
CS Sfaxien ya Tunisia
Espérance de Tunis ya Tunisia
ES Sétif ya Algeria
TP Mazembe ya Congo DR
Zamalek ya Egypt
Mechi za Makundi zitaanza Wikiendi ya Mei 16 hadi
18.
CAF Kombe la Shirikisho
Kwenye CAF Kombe la Shirikisho, Droo ya hapo
kesho Jumanne pia itashirikisha Timu 8 ambazo nazo zitagawanywa Makundi mawili
ya Timu 4 kila moja ambayo yatacheza mtindo wa Ligi, Nyumbani na Ugenini, ili
kupata Timu mbili za juu toka kila Kundi kucheza Nusu Fainali.
Timu hizo 8 ni:
Sewe Sport - Ivory Coast
Al Ahly – Egypt
AS Real de Bamako – Mali
AC Leopards de Dolisie – Congo
ASEC Mimosas Abidjan - Ivory Coast
Coton Sport FC – Cameroon
E.S. Sahel – Tunisia
0 comments:
Post a Comment