Tuesday, 29 April 2014

Uzoefu utatufanya sisi kuwa mabingwa-Zabaleta

Mchezaji wa Manchester City Pablo Zabaleta anaamini uzoefu wa Manchester City nyakati hizi za mwisho za ligi unaweza ukawawezesha kutwaa taji la Ligi ya Uingereza  sawa na walivyofanya 2012,imeelezwa na Supersports.com
Miaka miwili iliyopita, mabao mawili ya dakika za mwisho yalipelekea City kupata ushindi wa 3-2 dhidi ya Queens Park Rangers siku ya mwisho ya msimu na City wakatawazwa mabingwa wa Uingereza kwa mara ya kwanza tangu 1968, na kuwapiku mahasimu wao United kwa wingi wa mabao.
Baada ya kushuhudia City wakienda alama tatu kutoka kwa viongozi Liverpool, wakiwa na mechi moja waliyosalia nayo baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya  Crystal Palace Jumapili, Zabaleta anasema huenda historia ikajirudia tena msimu huu.
“Tunajua kwamba tumekuwa katika hali hii awali miaka miwili iliyopita na nafikiri tumekuwa tukiongea kuhusu hili wiki iliyopita,” alisema beki huyo wa City 
"Jambo muhimu zaidi tulilojifunza  ni kuwa na moyo wa kuendelea kupigana hadi mwisho.
“Yule atakayemaliza bingwa, ni kwa sababu anastahiki, na sisi ni moja ya timu hizo zitakazopigania taji hilo.
"Twatumai kwamba tunaweza kuendelea kushinda mechi na kuonyesha kwa mara nyingine kwamba wachezaji hawa, timu hii, meneja huyu, makocha hawa, bado wanafanya kazi kwa bidii na wanatamania sana taji hilo.”

0 comments:

Post a Comment