Thursday, 29 May 2014

Australia tayari imetua Brazil,ni nchi ya kwanza kufika kabla ya kombe la dunia 2014.

Timu ya taifa ya Australia imekuwa timu ya kwanza kuwasili nchini Brazil, huku zikisalia siku kumi na nne kabla ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 kuanza kutimua vumbi lake kwenye viwanja 12 tofauti,.
Australia wamewasili nchini Brazil katika mji wa Curitiba na watakaa hapo kwa siku kadhaa, kabla ya kuelekea kwenye mji wa Vitoria ambapo ndipo mchezo wao wa kwanza wa kundi la pili dhidi ya chile utakapochezwa July 13.
Socceroos wamewahi kuwasili nchini Brazil kwa lengo la kuendelea na kambi ya kujiandaa na fainali hizo, na pia watautuimia muda wa majuma mawili uliosalia kwa lengo la kuizoea hali ya hewa ya kusini mwa bara la Amerika.
Kiungo wa Socceroos ama timu ya taifa ya Australia Tommy Oar, amesema wamefurahishwa na mapokezi waliyoyapata kutoka kwa mashabiki waliojitokeza kuwalaki kwenye uwanja wa ndege wa Southern city, ambapo wanaamini huenda miongoni mwa mashabiki hao wakawa wafuasi wa kuwashangilia watakapoanza kampeni ya kuusaka ubingwa wa dunia.
Mbali na Chile ambayo itafungua michezo ya kundi la pili kwa kupambana na Australia, timu nyingine zilizopangwa kwenye kundi hilo ni mabingwa watetezi Hispania pamoja na Uholanzi.

0 comments:

Post a Comment