Thursday, 29 May 2014

Nile basin Cup robo fainali Merreikh na Tchite,Mbeya city na Victoria ya Uganda.

Mashindano ya kandanda ya kombe la Cecafa Nile Basin yanaingia robo-fainali Ijumaa na Jumamosi nchini Sudan huku timu mbili za Sudan, Al Merreikh na Al Shandy, na AFC Leopards ya Kenya zikiongoza makundi yao.
Al Merreikh na Victoria ya Uganda zilimaliza mechi zao za makundi na Alama saba kila mmoja lakini Merreikh ikaongoza kundi A kwa sababu ya wingi wa mabao.
Merreikh sasa itakutana na Academie ya Tchite Burundi ambayo Jumatano ilimeza bao 1-0 dhidi ya AFC Leopards ya Kenya, mfungaji akiwa ni Bernard Mangoli.
Victoria inapepetana na Mbeya City, Leopards dhidi ya Defence ya Ethiopia, Al Shandy inakwaruzana na jirani wao wa Sudan Kusini, Malakia.
Katika mechi za Jumatano, Leopards ilishangiliwa sana na baadhi ya wanafunzi wa Kenya wanaosomea Sudan pamoja na balozi wa Kenya nchini humo Abrown Suge na naibu wake Maurice Nakitare.

Etincelles imerudi nyumbani bila ushindi, na hawatasahu mechi yao ya mwisho dhidi ya Mbeya City waliposhindwa kufunga penalti, huku Al Shandy ikiicharaza Defence mabao 2-0, wafungaji wakiwa ni Nadir Eltyab na Omar Mahmoud.
Chanzo;BBC

0 comments:

Post a Comment