Gareth Bale aingia kwenye list ya waingereza waliotwaa mataji ya UEFA
Gareth Bale ameingia kwenye list ya majina ya wachezaji wa kiingereza waliotwa mataji ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya klabu yake ya Real Madrid kushinda mabao 4-1 dhidi ya Atletico Madrid mchezo uliomalizika kule jijini Lisbon Ureno jumamosi hii;Diego Godin aliipa klabu yake uongozi katika dakika ya 36 ya mchezo
Bale alifunga bao ambalo liliwapa nguvu Madrid katika mchezo huo baada ya kazi nzuri ya Di Maria kabla ya Marcelo na Cristiano Ronaldo kuongeza mabao mengine na kubeba taji ambalo wao wamelipa jina la La Decima
Kwa maana hiyo Bale anaungana na akina Paul Lambert na Steve McManaman, ambao walishinda mataji miaka ya 2000 baada ya Madrid kuifunga Valencia 3-0, katika wachezaji wa kiingereza waliotwaa mataji ya Ulaya na vilabu vya nje.
Kiungo wa zamani wa Manchester United Owen Hargreaves ni mchezaji mwingine wa Uingereza aliyeshinda UEFA na vilabu vya nje baada ya kuisaidia Bayern Munich kutwaa taji dhidi ya Valencia kwa mikwaju ya pelnati mwaka 2001.
0 comments:
Post a Comment