Sunday, 25 May 2014

QPR yarudi tena EPL,Zamora shujaa

Goli la dakika za lala salama la  Bobby Zamora limewarudisha Queens Park Rangers katika Ligi kuu Uingereza  Msimu ujao baada ya kuifunga Derby County Bao 1-0 kwenye Fainali ya Mechi za Mchujo za Daraja la Championship huku wakicheza pungufu kwa zaidi ya Dakika 30 za mwisho baada ya Kadi Nyekundu kwa Beki wao Gary O'Neil. QPR sasa wanaungana na Leicester City na Burnley kucheza Ligi Kuu Uingereza Msimu ujao.
 Vilabu vya Leicester City na Burnley, kwa kumaliza Nafasi za 1 na 2 kwenye Daraja la Championship, zilifuzu kucheza moja kwa moja Ligi Kuu Uingereza.
QPR na Derby zilifuzu kucheza Fainali hii baada ya kuzibwaga Wigan na Brighton kwenye Mechi za Awali zilizochezwa Nyumbani na Ugenini mapema Mwezi huu.
Mechi hizi za Mchujo zilihusisha Timu za Daraja la Championship zilizomaliza Nafasi za 3 hadi za 6 kwani Timu mbili za Juu ndio pekee hupanda Ligi Kuu Uingereza moja kwa moja.
Vijana hao wa Harry Redknapp wanarudi tena EPL baada ya kuporomoka  Daraja Msimu mmoja tu uliopita Mwezi Mei Mwaka Jana.

0 comments:

Post a Comment