Kazimoto awasili nchini tayari kuitumikia Stars
Kiungo mshambuliaji wa timu ya Al Markhiya ya Qatar,
Mwinyi Kazimoto amewasili nchini kujiunga na kikosi cha Taifa Stars
kinachojiandaa na mechi ya kufuzu michuano ya Afrika dhidi ya Zimbabwe.
Kazimoto ametua nchini jana ambapo kwa mujibu wa
taarifa ya Shirikisho la Soka nchini TFF iliyotumwa leo mchezaji huyo
ameshaondoka kwenda Tukuyu, mkoani Mbeya tayari kujiunga na timu hiyo iliyoweka
kambi yake huko chini ya kocha Mart Nooij.
Stars
ilicheza mchezo wa kirafiki wa maandalizi dhidi ya Malawi Jumapili iliyopita
ambapo walitoka sare ya bila ya kufungana mchezo ambao ulikuwa sehemu ya
maandalizi kwa ajili ya mechi hiyo dhidi ya Zimbabwe.
0 comments:
Post a Comment