Monday, 5 May 2014

Suarez abeba Tuzo nyingine

Mchezaji Luis Alberto Suárez Díaz wa Liverpool ametwaa Tuzo nyingine kubwa huko Uingereza baada kuteuliwa kuwa ndie Mchezaji Bora wa Mwaka wa, Chama cha Wanahabari wa  Soka,FWA (Football Writers' Association).
Suarez alizoa Kura Asilimia 52 na kuwabwaga Nahodha wake wa Liverpool, Steven Gerrard, na Yaya Toure wa Manchester City.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka ya FWA imekuwa ikiendeshwa kila Mwaka tangu Mwaka 1948.
Mwishoni mwa Mwezi uliopita, Suarez alitunukiwa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka na PFA, Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa (Professional Footballers' Association).
Tangu amalize Kifungo chake cha Mechi 10 alichopewa mwishoni mwa Msimu uliokwisha na kumalizika Msimu huu Mwezi Septemba, Suarez amewaka sana kwa kufunga Mabao 30 katika Mechi 31 na kuibeba Liverpool kwenye mbio za kuwania Ubingwa.
Suarez ni Mchezaji wa 7 katika Historia ya Ligi Kuu Uingereza kufunga Bao 30 katika Msimu mmoja.
Msimu uliopita, Gareth Bale, ambae sasa yuko huko Hispania na Real Madrid, wakati akiwa na Tottenham, ndie alietwaa Tuzo zote mbili za FWA na PFA.
Suarez, mwenye Miaka 27, atakabidhiwa Tuzo yake katika Chakula Maalum cha Usiku Jijini London hapo Mei  5 kwenye Lancaster London Hotel.

0 comments:

Post a Comment