Kikosi cha mwisho cha Hispania kuelekea Brazil
Kocha wa timu ya taifa ya Hispania Vicente del Bosque amemjumuisha mchezaji Diego Costa katika kikosi chake cha wachezaji 23 cha mwisho kwa ajili ya kombe la dunia kule Brazil ingawa mchezaji huyo ana majeraha.Nyota huyo wa Atletico Madrid ana tatizo la msuli na mchezo wa fainali ya UEFA dhidi ya Madrid alicheza kwa dakika 9.
Hispania wanataraji kuwa na mchezo wa kirafiki tena dhidi ya El Salvador mjini Washington DC siku ya June 7, kabla ya kuanza fainali za kombe la dunia.
Pamoja na Costa, Del Bosque pia amemjumuisha Fernando Torres wa Chelsea na David Villa, ambaye ndiye anashikilia rekodi ya ufungaji bora kwa upande wa Hispania.
Hakuna nafasi ya Jesus Navas, pamoja na mchezaji mwenzie wa Manchester city Alvaro Negredo.
Kikosi kamili: Makipa: Iker Casillas (Real Madrid), Pepe Reina (Napoli), David De Gea (Manchester United)
Walinzi: Sergio Ramos (Real Madrid), Gerard Pique (Barcelona), Raul Albiol (Napoli), Cesar Azpilicueta (Chelsea), Juanfran (Atletico Madrid), Jordi Alba (Barcelona)
Viungo: Xavi (Barcelona), Xabi Alonso (Real Madrid), Sergio Busquets (Barcelona), Andres Iniesta (Barcelona), Cesc Fabregas (Barcelona), Santi Cazorla (Arsenal), Koke (Atletico Madrid), Javi Martinez (Bayern Munich)
Washambuliaji: David Silva (Manchester City), Diego Costa (Atletico Madrid), Fernando Torres (Chelsea), Pedro (Barcelona), Juan Mata (Manchester United), David Villa (Atletico Madrid)
0 comments:
Post a Comment