Friday, 30 May 2014

Ballmer ainunua Clippers amshinda mshindani wake mkubwa Oprah Winfrey.

Mkurugenzi wa zamani wa Microsoft, Steve Ballmer, amefikia makubaliano na timu mashuhuri ya mpira wa vikapu ya Los Angeles Clippers ya kuinunua timu hiyo kwa dola billion 2,kwa mujibu wa CNN.
Ikumbukwe kuwa Sterling alitozwa faini ya £1.5mil. na pia amepigwa marufuku kuhusika kabisa na mchezo huo baada ya kashfa iliomkabili pale ilipoonekana kanda aliyorekodiwa akitoa matamshi ya ubaguzi wa rangi kuhusu wachezaji weusi wa mpira huo wa vikapu uliomaarufu sana Marekani.
Katika kushindania ununuzi huo ,Bw Ballmer aliwapiku wakinzani wake wawili akiwemo magwiji mahiri katika sekta ya vyombo vya habari akiwemo David Geffen na Oprah Winfrey.
Ballmer alistaafu kutoka Microsoft miezi mitatu iliyopita lakini bado ana kima kikubwa cha hisa katka kampuni hiyo zilizo na thamani ya zaidi ya dola billioni kumi na tatu.

0 comments:

Post a Comment