Soldado ruksa kuondoka Tottenham,Kroos anukia Old Traford.
Manchester United imekubali kutoa kiasi cha Euro milioni 25(Pauni milioni 20) kwaajili ya kumsajili kiungo wa Bayern Munich,Toni Kroos na wapo katika mipango ya kumnyakua winga hatari wa mabingwa hao wa Bundesliga na mchezaji anayefundishwa na Van Gaal katika timu ya taifa ya Uholanzi ,Arjen Robben.Tottenham Hostpus wao wameamua kumbakisha Emmanuel Adebayor lakini mpaka sasa hawajazungumza chochote na Mhispania Roberto Soldado
Mwenyekiti wa Klabu hiyo Daniel Levy amesema kuwa kama kuna klabu inamhitaji SWoldado wako tayari kuzungumza.
Klabu ya Barcelona ipo katika mipango ya kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich,Mario Mandzukic,raia huyo wa Croatia ameonekana pia kuwa kivutio kikubwa kwa timu za Chelsea,Manchester United na Arsenal zote kutoka Uingereza.
Liverpool wapo mbioni kumsajili mshambuliaji wa Barcelona,Pedro kufuatia klabu hiyo ya Uhispania kuwa tayari kumuachia nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 aondoke Camp Nou.
Pia klabu hiyo ya Anfield inajiandaa kupeleka ofa ya pauni milioni 18 kwa mshambuliaji wa Swansea City,Wilfried Bony huku ikimfukuzia na mlinda mlango wa klabu hiyo raia wa Uholanzi,Michel Vorm.
Mshambuliaji wa Lyon,Bafetimbi Gomis anataka dili la mshahara wa pauni laki 1(£100,000) kwa wiki ndipo aweze kukubali kujiunga na Newcastle United ya Uingereza.
Muingereza,Joleon Lescott anajiandaa kupata punguzo la asilimia 50 ya mshahara wake ili aweze kusalia katika ligi kuu ya Uingereza.
Beki huyo atakuwa nje ya mkataba na Manchester City majira ya joto huku akiwa anatakiwa na klabu za Aston Villa,West Ham na Hull City.
Meneja wa Liverpool,Brendan Rodgers yupo katika mbio za kutaka kumuhamishia Anfield beki wa kati wa Cardiff City,Steven Caulker.
Raia huyo wa Ireland anataka kuimarisha safu yake ya ulinzi mara baada ya kumaliza msimu wakiwa nafasi ya pili huku wakiruhusu wagoli mengi sana ya kufungwa katika ligi kuu ya Uingereza.
Chanzo;mtandao huu kushirikiana na mitandao mbalimbali ie Goal.com
0 comments:
Post a Comment