Thursday, 29 May 2014

Kinda wa Uholanzi akiri kuitamani Manchester United,amwambia wakala yu tayari kuondoka.

Winga wa klabu ya PSV Eindhoven Memphis Depay amemwambia wakala wake kuwa yuko tayari kujiunga na Manchester United ambao wameonesha nia ya kumsajili mholanzi huyo.
 Kocha mpya wa Manchester United  Louis van Gaal ni mshabiki mkubwa wa kijana huyo mwenye miaka 20  na amemtaja katika kikosi cha wachezaji watakaokwenda kombe la dunia nchini Brazil 2014.
Kwa mujibu wa gazeti la  Voetbal International, Depay amekubali mwenyewe kujiunga na klabu hiyo baada ya fainali za kombe la dunia.
Van Gaal anamhusudu kinda huyo. Vana Gaal mwenye miaka  62 alichaguliwa kuwa kocha wa Manchester United mapema mwezi huu na amekabidhiwa kiasi cha  £200 milion ili asajili.
Masheatani wekundau pia wameelekeza nguvu zao kumsajili  winga wa klabu ya   Dnipro Yevhen Konoplyanka, ambao wanacheza idara sawa uwanjani na Depay  ila  Depay anapewa nafasi kubwa ya kujiunga na  Manchester.

Van Gaal ambaye anaonekana kutaka kuwasajili wachezaji wengi wa Uholanzi baada ya tamati ya kombe la dunia anataka kuibadilisha klabu akiwa na malengo ya kubeba ubingwa katika msimu wake wa kwanza.
Wachezaji wawili wa  Feyenoord  Bruno Martins Indi na  Jordy Clasie  wanatajwa sana kujiunga na klabu hiyo sambamba na   Wesley Sneijder pamoja  Stefan de Vrij.

0 comments:

Post a Comment