Thursday, 29 May 2014

Kipa wa Arsenal akubali kujiunga na Swansea City, alipangua pelnati 2 kuelekea fainali ya FA

Golkipa wa klabu ya Arsenal  Lukasz Fabianski  amekubali kujiunga na klabu ya  Swansea City pindi mkataba wake utakapomalizika mwezi ujao.
Taarifa iliyoandikwa leo na mtandao wa klabu ya Arsenal  ni kwamba kipa huyo amekubali mwenyewe kujiunga na Klabu yake mpya inayotumia uwanja wa the Liberty.

"Kila mtu ndani ya  Arsenal  anamshukuru  Lukasz  kwa mchango wake ndani ya klabu yetu na tunamtakia maisha mema katika timu yake mpya," Imeeleza taarifa ya mtandao wa Arsenal.
Kipa huyo mwenye miaka  29 alijiunga na  Arsenal akitokea Legia Warsaw mwaka 2007 na amecheza michezo 78 katika mashindano yote.
Ingawa alionesha kiwango cha hali ya juu katika mafanikio ya Arsenal katika mbio zake za kutwaa kombe la  FA  msimu huu, Fabianski, aliyeokoa pelnati mbili katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya  Wigan haikumshawishi  Wenger kumtumia sana  na badala yake  Wojciech Szczesny  amebaki kuwa chaguo la kwanza.

0 comments:

Post a Comment