Thursday, 29 May 2014

Mmiliki wa Manchester United afariki dunia

Mmiliki wa Manchester United mmarekani Malcom Glazer ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 85 .
Taarifa ya mtandao wa Supersports imeeleza kuwa Mfanyabiashara huyo wa Marekani atakumbukwa kama bilionea wa Florida aliyeichukua kuimiliki binafsi United miaka tisa iliyopita na kuwekeza zaidi ya Pauni Milioni 500. 
  Mwenyenye  ambaye hakuwahi kufika uwanja wa Old Trafford kutokana na hofu ya kuwaudhi mashabiki wa timu hiyo ambao walikuwa wanamsuta kwa kupanga njama ya kuinunua klabu hiyo kwa kutumia madeni.
Kwa upande wa BBC imeeleza kuwa Glazer inasemekana alianza kisiriri kuwashawishi wenye hisa wa klabu hicho kumuuzia hisa zao tangu mwaka wa 2003 kabla ya kutwaa umiliki mwaka 2005.
United ambayo msimu uliopita ilitangaza faida kubwa ya asilimia 20 yaani pauni milioni 418 inakabiliwa na deni la zaidi ya pauni milioni 400.
Glazer aliyeugua kiharusi tangu mwaka wa 2006 amewawachia wanawe sita umiliki wa klabu hiyo ya Uingereza.
Msemaji wa United amesema: "Fikra za kila mmoja katika United zipo kwa familia,".
Familia ya Glazer bado wanamiliki Tampa Bay Buccaneers, timu ya mpira wa miguu ya Marekani waliyoinunua mwaka 1995. Na kwenye tovuti ya Bucs, ambako zimetangazwa habari za kifo cha Glazer.
Wakati wa umiliki wa Glazer, United imeweza kushinda mataji matano ya Ligi Kuu ya Uingereza na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Glazer ameacha mke, Linda waliyefunga naye ndoa mwaka 1961 na watoto na watoto sita, Avram, Kevin, Bryan, Joel, Darcie na Edward.

0 comments:

Post a Comment