Friday, 30 May 2014

Lambert kujiunga na Liverpool

Liverpool wanakaribia kumnasa mshambuliaji wa Southampton na Uingereza Rickie Lambert kwa Dau linaliodaiwa kuwa Pauni Milioni 4 .
Inatarajiwa Lambert atamaliza kupimwa Afya yake Jumapili kabla Kikosi cha England hakijaruka kwenda Miami huko Marekani kupiga Kambi yao ya mwisho kabla kuelekea Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Mwezi Januari, Southampton iligomea Ofa ya West Ham kumnunua Lambert lakini safari hii inaelekea wamekubali mshambuliaji  huyo mwenye Miaka 32 kuhama.
Southampton waliikata Ofa ya awali ya Liverpool kakini sasa mazungumzo baina yao yapo hatua nzuri na yanaelekea atamalizika kwa kuafikiana.
Lambert alikaa Miaka Mitano huko Anfield akiwa Chuo cha Soka kabla hajatemwa akiwa na Miaka 15 lakini bado ni Mpenzi wa Liverpool hadi hii Leo.
Mbali ya Lambert, Liverpool pia wanaongea na Southampton ili wamchukue Kiungo wao, Adam Lallana, mwenye Miaka 26, ambae yuko Kikosi cha England hivi sasa.

0 comments:

Post a Comment