U15 Tanzania Yashika nafasi ya pili AYG
Taarifa ya TFF kupitia afisa habari wake Boniface Wambura imeeleza kuwa Mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa SSKB
jijini Gaborone ambapo kwa matokeo hayo Tanzania imetwaa medali ya fedha
baada ya kushika nafasi ya pili. Nigeria ndiyo ilishika nafasi ya
kwanza na kutwaa medali ya dhahabu.
Tanzania imemaliza ikiwa na pointi kumi ambapo ilishinda mechi tatu, sare moja na kupoteza moja mbele ya Nigeria.
Katika mechi ya kwanza ilitoka sare ya
bao 1-1, ikawafunga Botswana 2-0, Swaziland wakachapwa 3-0 na baadaye
kuwafunga Afrika Kusini 2-0. Timu ya Tanzania inayofundishwa na kocha
Abel Mtweve ilifungwa na Nigeria mabao 2-0.
Wachezaji 16 waliounda kikosi hicho cha
Tanzania katika michezo hiyo inayomalizika leo (Mei 30 mwaka huu) ni
Adam Shayo, Amani Ally, Amos Manguli, Amri Nyuki, Amede Amani, Baraka
Rashid, David Uromi, Goodlove Mdumule, Hance Msonga, Kelvin Kamalamo,
Makalius Amrin, Nasson Chanuka, Paulo Ngowi, Petro Shaban, Rajab Mohamed
na Thomas Chindeka.
Nchi nyingine zinazoshiriki michezo hiyo
kwa upande wa mpira wa miguu ni Afrika Kusini, Botswana, Nigeria, Mali
na Swaziland wakati Gabon na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC)
zilijitoa dakika za mwisho.
0 comments:
Post a Comment