Ligi ya mabingwa Wa mikoa kuanza kesho,Tabora kuwakilishwa na Milambo
LIGI ya
Mabingwa wa Mikoa (RCL) inayoshirikisha timu 27 inaanza kutimua vumbi kesho
(Mei 10 mwaka huu) katika vituo vitatu vya Morogoro, Mbeya na Shinyanga kwa
mechi mbili kila siku.
Kundi A ambalo
mechi za
ke
zinachezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, African Sports ya Tanga itacheza
na Kiluvya United FC ya Pwani saa 8 mchana wakati saa 10 jioni ni Mji Mkuu FC
(CDA) ya Dodoma dhidi ya Pachoto Shooting Stars ya Mtwara.
Jumapili (Mei
11 mwaka huu) katika kundi hilo kutakuwa na mechi kati ya Bulyanhulu FC
(Shinyanga) na Kariakoo SC (Lindi) itakayoanza saa 8 mchana wakati saa 10 jioni
ni Navy FC (Dar es Salaam) na Abajalo FC pia ya Dar es Salaam.
Kundi B katika
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya litaanza ligi kwa mechi kati ya
Ujenzi (Rukwa) na Volcano FC (Morogoro) saa 8 mchana wakati saa 10 jioni ni AFC
ya Arusha na Panone FC ya Kilimanjaro.
Mei 11 mwaka
huu saa 8 mchana ni Mpanda United ya Katavi na Magereza ya Iringa wakati
Tanzanite (Manyara) na Njombe Mji (Njombe) zenyewe zitaumana kuanzia saa 10
jioni.
Simiyu United
ya Simiyu na Mvuvumwa FC (Kigoma) ndizo zitakazoanza kucheza saa 8 mchana
katika kundi C linalotumia Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Saa 10 jioni ni
mechi kati ya Wenda FC ya Mbeya na mabingwa wa Mkoa wa Kagera, Eleven Stars FC.
Jumapili (Mei
11 mwaka huu), mechi za kundi hilo zitakuwa Singida United (Singida) na Mbao FC
ya Mwanza kuanzia saa 8 mchana wakati jioni ni pambano kati ya mabingwa wa Mkoa
wa Mara, JKT Rwamkoma FC na Geita Veterans FC ya Geita.
Ligi hiyo
itamalizika Juni 2 mwaka huu ambapo timu itakayoongoza kila kundi itapanda
daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015.
Ikumbukwe
kuwa timu ya Milambo SC ya hapa mkoani Tabora imepangwa katika
kituo cha Shinyanga kwenye Uwanja wa Kambarage sambamba na ,Timu za Eleven
Stars ya Kagera, Geita Veterans (Geita), JKT Rwamkoma FC (Mara), Mbao FC (Mwanza),
Mvuvumwa FC (Kigoma), Simiyu United (Simiyu), Singida United (Singida) na Wenda
FC (Mbeya)
0 comments:
Post a Comment