Nitatetea kwa mara ya 5 kiti cha urais-Blatter
RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp
Blatter ametoa dokezo lingine kuwa amepanga kutetea kiti chake hicho kwa mara
ya tano katika uchaguzi wa shirikisho hilo mwaka ujao.
Blatter alikaririwa na gazeti la nchini Uswis akidai
kuwa anataka kufanya hivyo kwasababu anaona bado hajamaliza.
Gazeti hilo liliendelea kumkariri rais huyo akidai
kuwa uongozi wake unafikia kikomo lakini mipango yake aliyoweka bado
haijakamilika. Blatter mwenye umri wa miaka 78 alichaguliwa bila kupingwa
katika kipindi chake cha nne mwaka 2011 baada ya mpinzani wake Mohamed Bin
Hammam kujitoa baada ya kutuhumiwa kutoa rushwa ili aweze kupigiwa kura hatua
ambayo ilipelekea kiongozi huyo kufungiwa maisha baadae.
Rais huyo aliwahi kusema kwamba kipindi hiki
kitakuwa cha mwisho kwake lakini Februari mwaka huu alibadili mawazo hayo na
kudai kuwa anajiona yuko katika afya njema hivyo haoni sababu ya kishindwa
kufanya kazi na kama akihitajika kugombea hatakataa wito huo.
0 comments:
Post a Comment