Zaneti aagwa rasmi na Inter,Juve na Roma leo
Huku mashabiki wakishuhudia gwiji na beki wa kimataifa wa Argentina Javier Zaneti akiwaaga mashabiki wa Inter Milan mabingwa wapya wa Serie A huko Italia, Juventus, ambao Wiki iliyopita walitetea vyema Taji lao wakiwa na Mechi 3 mkononi, leo jumapili Usiku wako Ugenini Stadio Olimpico kucheza na Timu ambayo imetwaa Nafasi ya Pili, AS Roma.Kocha wa AS Roma, Rudi Garcia, licha ya sasa kutokuwa na Nafasi tena ya kuiporomosha Juve, ametaka Timu yake icheze kwa ari na furaha ili kuaga Mashabiki wao kwenye Mechi hii ya mwisho Uwanjani kwao kwa Msimu huu.
Ikiwa AS Roma wataifunga Juve, hii itamaanisha wamezifunga Timu zote 19 za Serie A Msimu huu.
Garcia amesema: “Msimamo wa Ligi ndio huo, Juve wa Kwanza, Roma wa Pili lakini tuliwafunga Juve kwenye Coppa Italia na wao walitufunga kwenye Ligi huko kwao Turin!”
AS Roma wataingia kwenye Mechi hii wakimkosa Kipa wao Morgan De Sanctis ambae amechubuka mkono na badala yake atacheza Kipa wa Miaka 23 kutoka Poland, Lukasz Skorupski.
Juventus itawakosa Arturo Vidal, Sebastian Giovinco na Mirko Vucinic.
Baada ya kuitumikia klabu ya Inter milan ya Italia kwa miaka 19 hatimaye nahodha na mlinzi wa klabu hiyo Javier Zaneti amestaafu na kuagwa rasmi na mashabiki,viongozi na wachezaji wa klabu hiyo ktk mchezo dhidi ya lazio uliomalizika kwa Inter kushinda 4-1....amecheza mechi 857 na kufunga mabao 12.....amekuwa nahodha tokea Mwaka 1999-2014..

0 comments:
Post a Comment