Listi ya wachezaji 20 bora wadogo wanaong'ara Ulaya,Pogba balaa
Kiungo wa klabu ya Juventus Paul Pogba amewashinda akina Thibaut Courtois na Kurt Zouma baada ya kutajwa kuwa mchezaji bora nyota katika wale wachezaji wadogo ambao wanaendelea kung'ara barani Ulaya.Kwa mujibu wa gazeti la Daily mail iliyotolewa hii leo ni kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United ametoa msaada mkubwa kwa klabu ya Juventus kutwaa ubingwa wa Italia msimu huu na mapema mwaka huu alipata tuzo ya Golden Boy.
Pogba aliondoka Old Trafford mwaka 2012 akilalamika kukosa namba ndani ya kikosi cha Ferguson wakati ule lakini kwa sasa Manchester United inasemekana watahitaji kumrudisha tena Uingereza.
Mchezaji huyo mwenye miaka 21 alifuatwa kwa karibu na kipa wa Chelsea Thibaut Courtois, ambaye kwa sasa anadakia Atletico Madrid kwa mkopo.
20 BORA WACHEZAJI WADOGO WANAONGA'ARA ULAYA
20. Stephan El Shaarawy (Milan)
19. Paulo Dybala (Palermo)
18. Ali Adnan (Rizespor)
17. Alvaro Vadillo (Real Betis)
16. Zakaria Bakkali (PSV)
15. Mattia de Sciglio (Milan)
14. Kurt Zouma (St Etienne/Chelsea)
13. Hakan Calhanoglu (Hamburg)
12. Marquinhos (PSG)
11. Viktor Fischer (Ajax)
10. Jese Rodriguez (Real Madrid)
9. Marco Verratti (PSG)
8. Julian Draxler (Schalke)
7. Florian Thauvin (Marseille)
6. Ricardo Rodriguez (Wolfsburg)
5. Lucas Moura (PSG)
4. Raphael Varane (Real Madrid)
3. Mario Gotze (Bayern Munich)
2. Thibaut Courtois (Atletico Madrid)
1. Paul Pogba (Juventus)
0 comments:
Post a Comment