Timu ya soka ya Tanzania Taifa stars itaondoka kesho alfajiri (Mei 29 mwaka huu) kwenda Harare, Zimbabwe kwa ajili
ya mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika.
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF kupitia msemaji wake Boniface Wambura,Mechi hiyo itachezwa Juni Mosi mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa mjini Harare-
na Taifa Stars itatua jijini humo saa 5 asubuhi kwa ndege ya Kenya Airways.
Stars itaondoka na Msafara wa watu 30 unaojumuisha wachezaji, benchi la ufundi na viongozi
Timu hiyo ambayo jana (Mei 27 mwaka huu) ilicheza mechi ya
kujipima nguvu na Malawi na kushinda bao 1-0, na itarejea nchini Juni 2 mwaka
huu na msafara unaongozwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi
Wakati
huo huo, mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars na Malawi (Flames) iliyochezwa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 8,380,000 kutokana na watazamaji
1,504 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo.
Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh.
1,278,305.08, gharama za kuchapa tiketi sh. 225,600, gharama za uwanja sh.
1,031,414.24, gharama za mechi sh. 1,375,218.98 na TFF/Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) sh. 4,469,461.69.
0 comments:
Post a Comment